Jumanne 17 Februari 2026 - 17:30
Malaysia yafanya kikao cha kusoma na kuhifadhi Qur’ani katika ngazi ya baraza la mawaziri

Hawza/ Kikao hicho cha Qur’ani katika ngazi ya serikali kiliandaliwa na Waziri Hajiji Noor na kilipokelewa kwa mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi wa Malaysia. Waziri huyo alieleza kuwa, hatua hiyo ni juhudi ya kuimarisha ustawi wa kimaadili na kiroho wa jamii ya Malaysia.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Waziri Datuk Seri Hajiji Noor alisema kuwa; mkutano wa kusoma na kuhifadhi Qur’ani katika ngazi ya baraza la mawaziri ni miongoni mwa mipango ya kimkakati ya serikali ya jimbo kwa ajili ya kuwahamasisha Waislamu na kuenzi nafasi tukufu ya Qur’ani.

Hajiji alisisitiza kuwa, kuendelea kuandaa tukio hili la kidini kila mwaka kunaonesha dhamira ya serikali ya Malaysia ya kuhakikisha maendeleo yaliyo na uwiano kati ya ustawi wa kiroho na maendeleo ya kimwili, ili kufikia maelewano kati ya maendeleo ya kidunia na ustawi wa kimaadili na kiroho katika jamii ya Malaysia.

Aliongeza kuwa; mkutano huo ni jukwaa la kuzalisha wasomaji na wahifadhi bora wa Qur’ani watakaotukuka katika usomaji na hifdhi ya Qur’ani, na wakati huo huo kuwa mfano wa uongozi wa kijamii kwa wananchi.

Chanzo: Daily Express

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha